OwlTail

Cover image of Salama Na

Salama Na

‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama na, Salama gets to sit down for exclusive chats with Celebrities, Influencers and Change makers in the society. Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Weekly hand curated podcast episodes for learning

Popular episodes

All episodes

Read more

‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama na, Salama gets to sit down for exclusive chats with Celebrities, Influencers and Change makers in the society. Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Ep. 55 - Salama Na PROFESA | MAPINDUZI HALISI

Podcast cover
Read more

SALAMA NA PROF JAY

---

Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Feb 25 2021

1hr 27mins

Play

Ep. 54 - Salama Na VANNY BOY | NDAGHA

Podcast cover
Read more

Kutoka kwao Mbeya mpaka Dar es Salaam kwaajili ya kutafuta maisha bora na maendeleo kama wengi wetu ndo ilikua nia na madhumuni ya Raymond wa enzi hizo. Ingawa kuna kipindi ilifika alikua hataki kabisa kuskia habari za muziki, ila alipoambia kama kuna pesa ndani yake katika huo mchongo wa mashindano ambayo aliitiwa na akiangalia nyumbani moja haikai na mbili haijulikani ilipo akaona basi sawa, kwani nini? Na huo ndo ulikua mwanzo wa safari nzuri ya ki superstar ambayo anaishi nayo sasa.

Najua wengi wenu mlikua mnadhani labda yangezungumziwa madhila alokua nayo sasa ila kwa bahati mbaya (kwako) na nzuri kwetu, sisi tulizungumza naye kabla. So hii ilikua free na natural kama ambayo utaiona au kuiskiliza. Wengi wetu huwa tunapitia madhila na mitihani mingi tu kabla ya kujielewa na kusimama sawa sawa, na kupitia hayo ndo kujifunza na kuwa BORA kunatokea. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili unaoenda kama, ‘asipo chafuka, atajifunzaje’, something like that.

Mimi Ray huyu nilianza kumsikia vizuri zaidi kutoka kwa AY ambaye ali spend naye muda mwingi hapa Bongo wakati wanafanya rekodi remix ya Zigo na nchini Afrika ya Kusini wakati Zee ameenda ku shoot video ya wimbo huo ambao Diamond Platnumz ndo ameshirikishwa, ila Vanny Boy alikuwepo all the way na mpaka kwenye video akatokea. AY aliniambia kuhusu ucheshi wake na uhodari wake, na uhodari huo ameuzungumza humu kwenye maongezi yetu mimi na yeye. Aliniambia jinsi ambavyo alikua akitumia kipaji chake enzi hizo kwa kuwaandikia wenzake wimbo mmoja na pengine mpaka album kwa shilingi ELFU THELATHINI TU.

Njia ambazo watu wengi wamepita haiwezi kuwa ndo njia ambayo kila mmoja wetu atapitia pia, ila kunaweza kuwa na mifanano ya hapa na pale, na hii ndo nia na madhumuni ya kipindi hiki. Tunataka wewe usikie na ujifunze ili ujue ‘unatokaje’ au watu walipenya vipi mpaka wakafika!

Sasa ni mmoja ya wasanii wakubwa tu hapa barani Afrika na duniani anafahamika. Bango la album yake linaning’inia kwenye mitaa ya Times Square huko NY City kwenye mji ambao raia wa nchi mbalimbali duniani wanaishi na kupitia. Sidhani kama wakati anahangaikia kufua nguo zake zilizomwagikiwa mafuta ya mawese wakati akiwa safarini kwenye lori kutoka Mbeya kuja Dar aliwahi kuwaza jambo kama hilo.

Mimi na yeye tulizungumzia pia mahusiano yake na wazazi wake, familia ya kufikia ya Baba yake ambaye aliachana na Mama yake na kuhamia na mtu mwengine si mbali na wao walipokua wanakaa. Tumeongelea mapenzi yake na muziki na kipaji chake cha uandishi. Tumeongelea jinsi ambavyo Madee alimpokea na Babu Tale ambavyo alikua na kama kusita hivi kwenye suala la yeye kusajiliwa WCB na mambo mengine mengi ya maisha. Yangu matumaini kama ilivyo ada, hapa utajifunza jambo pia.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

---

Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Feb 18 2021

1hr 14mins

Play

Ep. 53 - Salama Na NANDY | MNOGESHAJI

Podcast cover
Read more

Huyu si moja ya marafiki zangu, as in si Mtu amable nafahamiana naye sana, ambaye nishawahi kukaa naye muda mrefu na kupiga story, au kusafiri naye au kuwa studio wakati anafanya mambo yake au namjua mzazi wake au mtu wake wa karibu kwenye familia yake ila nawajua watu ambao wanamfahamu kwa ukaribu na watu hao ndo ambao walinipa mimi mawazo ya kutaka kumfahamu vizuri binti huyu hodari wa ki Tanzania bila ya hata ya wao kujua.

Baadhi ya Dada zangu walifahamiana naye kwenye kipindi cha msiba wa Marehemu Ruge Mutahaba, kipindi hiko kilikua cha masikitiko kwao na kwake pia. Nandy alikua na ukaribu mwingi na Ruge, alishawahi kumtembelea hospitali mara kadhaa na pia alikua na mawasiliano ya moja kwa moja na watu wa karibu wa familia kipindi kile ambacho Ruge alikua hana tena mawasiliano naye moja kwa moja. Siku ambayo Ruge alitangulia muelle ya haki, muda si mrefu kabla ya hilo halijatokea Nandy ananiambia alizungumza na nesi wa zamu siku hiyo na pia alimuekea simu kwa ukaribu na alimsikia akiwa anapumua. Wapi alikua wakati anapata habari hii iko kwenye maongezi yetu haya, humu pia utaelewa connection ambayo sisi binadamu tunayo na watu ambao tunawapenda na wanao wanatupenda.

Najua siku hazigandi kama ambavyo Lady Jd alishawahi kuimba na ndo  nikawaza, hivi ushawahi kuwaza Nandy amekua kiasi gani toka msiba wa Ruge utokee? Unakumbuka baadhi ya maneno yalosemwa juu ya career yake baada ya msiba ule? Tunafahamu kwamba alipoteza rafiki, mentor, baba na kama tochi yake? Mimi huwaza haya sana, na hilo la yeye kujidhatiti na kukaza mwendo ndo ambalo lilifanya mimi binafsi niseme you know what, it’s time.

Nandy ni MPAMBANAJI, anaupenda muziki na kama mtu mwengine yoyote mwenye jitihada basi Mungu humfungulia milango ya Kheri. Kaniambia humu kwenye mangezi yetu kwamba safari yake ya kwanza kwenda nchini Nigeria kwenye mashindano ya kuimba alimuambia Mama yake wakati yumo ndani ya ndege, alipomaliza hutuba yake fupi alizima simu na wheels up, to Lagos ambako alihakikisha anapigana mpaka fainali na kumaliza nafasi ya tatu. Si kitu kidogo kwa binti ambaye aliamua kuweka shule pembeni ili atimize ndoto yake, ndoto ambayo hata Mama yake mzazi hakua na taarifa nayo.

Siku zinakwenda, maisha yanasonga na yeye ameendelea kukimbiza ndoto yake na mpaka tunaenda mitamboni, Nandy ni mmoja wa wasanii wa kike wakubwa sana hapa nyumbani na barani Afrika na hata Ulaya na Marekani na ukitizama vizuri utajua kwamba huu ni mwanzo tu wa mazuri ambayo yatatokea katika maisha yake. Mimi na yeye tulizungumzia mahusiano hayo pamoja na kukimbiza ndoto zetu. Tuliongelea Bill Nas na kiwanda cha muziki wa Bongo Flava. Tuliongelea muziki wake na collabo ambazo amewahi kufanya. Hapo hapo nilitaka kujua pia yeye ni mtu wa aina gani na ni vitu gani vinamsukuma kutaka atake zaidi na sehemu ambayo anajiona huko mbeleni In Shaa Allah.

Yangu matumaini kama kawaida ni kwamba utajifunza mawili matatu ambayo yatakusaidia kupambana na mitihani ya maisha kwasababu tu umejifunza kutokana na sehemu wenzetu hupitia kwenye maisha yao.

Tafadhali Enjoy.

Love,

Salama.

---

Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Feb 11 2021

1hr 4mins

Play

Ep. 52 - Salama Na HAJI | ALIYE KUTWIKA NDIYE ATAKAYEKUTUA

Podcast cover
Read more

Haji Sunday Manara nlitaka kusema ni rafiki YANGU ila vacati navaza hilo nikakumbuka mmh, Haji Sunday Manara ni rafiki wa WATU WENGI hususan mashabiki wa klabu wangu pendwa na zaidi kwa watu ambao hawapendi hata mpira ila wanampenda tu jinsi anavyoseti mambo yake na anavyoigeuza sehemu yoyote aendayo kama sehemu yake ya kujitamba na kujitutumua na tofauti yake na WACHACHE ambao wanafanya kazi kama yake ni kwamba yeye anaweza KUYATEMBEA yale anayo YAONGEA.

Mapenzi yangu kwake ni ya first class na namini hata yeye analifahamu hilo, huwa namtazama kwa kuvutiwa hasa kwababu ya anavyojibeba na kukiaminisha kile ambacho anakisema, iwe kuhusu Simba, bidhaa ambayo anaitangaza au hata simulizi za maisha , vyovyote vile vitakufanya utake kumskiliza kwa umakini, na pia ni lazima ucheke. Utashi wake kwenye mambo mengi pia ni jambo la kupendeza, ukiniuliza mimi nitakuambia sawa, hata kama ni mtoto wa Kariakoo, ni watoto wa Kariakoo wangapi ambao wewe unawajua wana kipaji cha kuongea na kumfanya mtu ajiskie kama ambavyo Haji anafanya baadhi ya watu wajiskie? Iwe kwa kuzodoa au kusifia wangapi? Maneno ya papo kwa papo au hata ya kujindaa (hapo ndo utachoka kabisa), yupi?

Urafiki wetu ulianzia pale kwenye USIMBA DAMU na tuli click tu moja kwa moja, niliamini timu wangu ido kwenye mikono salama kabisa kama jina langu, tufungwe atasema maneno ya kutufanya tunyoshe mgongo na kusimama vuzuri na tukishinda well tukishinda mziki unaufahamu vizuri tu, na tukisajili je? Ahaha… Huyu mtu huya ananipa raha sana, Nba hiyo neo ilikua sababu ya Mimi na wenzangu kumvuta kitini.

Maneno mengi yamekua yakisemwa juu yake na pia mdomo wake huo ulishawahi kumtia matatani kipindi flani kile ambacho Bwana Mo Dewji alipopata matataizo, si unakumbuka? Haji alitiwa ndani siku kadhaa mpaka alipokuja kuwa cleared kwamba hakua anahusika, sikuongea nae kuhusu hilo kwasababu tu za kutotaka asiwe comfy kwenye kiti chetu ( ingawa najua ningeuliza asingekua na hiyana hata). Maneno mengine ni kuhusu urafiki wake na matajiri wa mjini ambao wengine ni wamiliki wa time pinzani za muajiri wake, hili likoje? Huwa anasumbuka wananchi wanapolileta kwenye comments za ukurasa wake maarufu wa Intagram?

Mzaliwa wa Udachini kule nchini Holland, Haji amekua hapa Dar es Salaam kwa malezi ya Bibi na Babu zake maana kipindi hicho Mzee wake alikua anakipiga nje zaidi, mimi nilitaka kujua hiyo historia yake na mpira na Mzee wake, Yanga (ambayo tunaweza kusema ni team ya familia), elimu yake na mambo ya ndoa na scandal za mitandaoni za hapa na pale. Pia tuliongelea pale alipokua wakati shabiki wa Simba Bwana Hamisi Kingwangalla alipohoji uwekezaji wa Mo Dewji na bilioni 20 za uwekezaji, na mano yake hasa kuhusu hiyo situation.

Nimecheka sana, nimeskiliza sana, nime admire sana na zaidi nimejifunza mengi ambayo nilikua siyafahamu kuhusu mtu huyo maalum na tunu ya Taifa hili. Yangu matumani utaelewa na kujifunza jambo hapa.
Tafadhaki enjoy rafiki.

Love,
Salama.

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Feb 04 2021

1hr 23mins

Play

Ep. 51 - Salama Na Babu Tale | JUGGLER

Podcast cover
Read more

Hamis Tale Tale ni MWAMBA wa maisha yake na ya wale walomzunguka kwa miaka nenda miaka rudi na kutoka upande huu wa muandishi na mtangazaji ni heshima tu kwenda mbele. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili kuhusu nyani ambaye unamkuta mjini. Ya kwamba anakua kashakwepa MISHALE ya kutosha kwahiyo unapomkuta town inabidi umpe heshima zake za kutosha.

Kwa waasisi wa Bongo Flava jina lake kuwa juu pale na haiwezi kuwa kosa hata kidogo na kuna wasanii kibao ambao wana mshutumu kwa mambo mengi lakini kuna wale ambao hawawezi kumsahau maishani mwao kwa sababu ya mchango mkubwa ambao amewapa. Na vile vile ukimtaka mtu wa kukuelezea tabia na uzuri wa watu wa iaina zote katika industry hii basi Babu Tale ndo ambaye atakuelezea hilo kwa kinaga ubaga maana akiachana na ucheshi wake, Tale pia ni msimuliaji habari mzuri tu.

So kuanzia kwa Marehemu Kaka yake Abdu Bonge mpaka kwa huyu anayevaa kaunda suti zilizonyooka ndo sisi tulipopataka, ametoka umbali gani? Haya yote aliyonayo ilikua ndo mipango yake? Ki ukweli mmoja kama anaamini ya kuwa kuna yatu wanakua wamekaa tu wanaangalia progress zeta kwa mbali na kuona haswa umbali gani watu wametembea mpaka kufika kwa mfano ambapo Tale amefika basi bila ya shaka atakua ametia nne yake huku akiwa kapendeza sana na kumpigia makofi tu kwa yale aliyoweza kuyafikia mpaka sasa. Ukichukulia huyu ni Kijana ambaye kuna wakati flani katika maisha yake ilikua inabidi asubiriane na mmoja ya ndugu zake ili waweze kubadilishana aidha viatu au uniform ili na yeye aweze kwenda shule!

Nimekutana na watu wengi  katika maisha yangu na Tale yeye yake tabia ni kutokua na breki pale anapokua na lake, yale mambo ya sijui kulainisha maneno ili pengine asikuumize hisia zako yeye hana, kinda like me, la kusemwa lisemwe kisha maisha yaendelee, na hiyo ni kwa kumtakia mtu mema tu, pia anachekesha na anapenda kucheka pia, also… Mkali, sio wa ‘kulealea’, sio babysitter hata kidogo na hiyo yote ni kwa kutaka JEMA kwa mtu ambaye anamsimamia. Najua kama binadamu atakua na mapungufu yake na hayo ndo yako pia kwenye maneno ya baadhi ya wasanii ambao ameshawahi kufanya nao kazi.

Tale ana khadithi ya kila mmoja wetu kwenye kiwanda hiki cha muziki na burudani na nna uhakika miaka kadhaa ya mbele atakua na khadithi za wanasiasa wenzake na viongozi ambao kuanzika mwaka huu anaanza kuwa nao kwa muda mrefu kwenye maisha yake.

Mwaka jana Babu Tale alimpoteza mke wake kipenzi ambaye alitangulia mbele ya haki na kumuachia watoto ambao sasa yeye ndo anaye waangalia kwa msaada pia wa baadhi ya ndugu zake. Hii ilikua habari nzito kwa kila mtu, mke wake amble wengi tulikua tunamfahamu zaidi kupitia mitandano ya kijamii, mimi nishawahi kukutana naye mara kadhaa, alikua Mrembo sana wa sura na roho, Mwenyezi Mungu Amrehemu. Mengi sana yalisemwa na kwa ufahamu wangu nikaona basi hakuna wa kutuambia ambayo tunadhani tuna haki ya kuyajua zaidi yake YEYE. Nini haswa kilitokea?

Natumai maongezi yetu haya yatakupa somo flani kwa mambo kadhaa ambayo tunakutana nayo maishani mwetu, Tale amanitajia watu ambao kwa kiasi kikubwa wanamsaidia kumpa faraja baada ya mkewe kutangulia mbele ya haki, na watu hao hata sio NDUGU ZAKE, ingawa najua nao kwa kiasi chao wanamsaidia ki vyao. Hili kwangu liliingia haswa.

Humu kuna mengi tuliyagusia na hakua na hiyana kutuambia mawazo yake na kwa hilo napenda kumshukuru. Tafadhali enjoy session hii ambayo kama kawaida natumai itakufunza mambo mawili matatu, iwe kuhusu mapenzi, maisha, kazi, watoto, muziki, marafiki na hata siasa, Na pengene hata jinsi ya kukimbiza naoto zako!

Love,
Salama

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Jan 30 2021

1hr 16mins

Play

Ep. 50 - Salama Na SUGU | UJIO WA UMRI

Podcast cover
Read more

Turudi nyuma mwaka 1999 wakati nilipomaliza kidato cha nne kwahiyo nilikua sina mitkasi mingi zaidi ya kumkimbia Mama inapofika mchana ili niende kucheza zangu basketball pale Msasani kiwanja cha Pazi. Nlikua natokea zangu Mbagala Charambe nachukua zangu basi mappa Mbagala Rangi tatu then muunganisho unaendelea mpaka nafika zangu mazoezini, nilifanya urafiki na makonda na madereva weeengi kiasi kwamba nilikua ‘staff’ kwenye daladala nyingi, na huwezi kuamini nyingi pia nilikua nikiingia basi radio nlikua namiliki MIMI. Station gani tunaskiliza au tape gani tunaweka ili safari inoge na muziki. Nakumbuka jinsi ambavyo Sugu alikua anaikosha, anakosha nafsi yangu na ya abiria wote ambao walikua wanasafiri nasi basi moja. Chini ya miaka 18 ilikua inaongea na mimi haswam inanifanya nisitake kuwa yule binti ambale Sugu alikua namuongelea ASILAN! Mikononi mwa Polisi… Album kali kama Nje ya Bongo, Millenium, Muziki na Maisha zilifuata na wakati hizi nyengine zinatoka nami tayari nilishaacha kumtia wasiwasi Mama yangu wa kurudi nyumbani usiku na kuwa DJ wa muda ndani ya Daladala za Mbagala Posta au Mbagala Kariakoo na kuweza kupata kazi yangu ya kwanza pale Times FM kabla sijajiunga na EA Radio na TV.

Mapenzi yangu kwa Sugu na muziki wake yako wazi na naamini na yeye anajua maana huwa namuambia kila tunapokutana, pia napenda kuwa around na yeye maana confidence yake ni kitu cha kujifunza. Haogopi, anajiamini na uthubutu wake katika mambo yake mengi ni jambo ambalo wengi wetu tunajifunza sana kutoka kwake. Kuanzia jinsi alivyokua anajibeba, mapinduzi ya uandishi na muziki ambayo amefanya na anaendelea kufanya mpaka leo hii ni kitu ambacho kama utakua unamfuatilia kwa karibu basi utakua huna la kufanya zaidi ya kupenda jinsi anavyofanya mambo yake.

Siku zote nimekua nikitaka saaana kufanya nae interview lakini kama tujuavyo, Mungu ndo mpangaji wa yote na round hii ilikua ndo wakati muafaka. Nilimcheki naye akakiambia kwamba Mimi ni mtu pekee ambaye angependa aongee naye so mengine yakawa historia tu.

Brother alikuja Dar es Salaam malum kabisa kwaajili ya kuongea na sisi na kwa hilo tunamshkuru sana. Mambo ya kisiasa yalikua sio focus yetu hata kidogo na badala yake tulitaka kumfahamu yeye zaidi na pengine mmoja anaweza kujifunza kwa kufuatilia tu nyenendo zake kwenye mitandao.

Kaka alishawahi kwenda jela, amempoteza Mama yake kipenzi pia muda si mrefu baada ya yeye kutoka. Sisi tuliongea naye kuhusu mapenzi yake na Mama yake kipenzi Desderia ambaye hata jina la hoteli yake ameipa jina la Mama yake. Nilitaka kujua ukaribu wao huo ulitokana na nini, jinsi ambavyo Mama alimpa support kipindi hicho ambacho muziki ulikua unaonekana kama uhuni tu. Maoni yake kwenye masuala mbali mbali na kuhusu urafiki na mafanikio. Pia nilitaka kujua historia yake ya muziki na njia alizowahi kupita. Mambo mengine ni kuhusu suala la yeye kuwa Baba na mapenzi kwa ujumla.

Yangu matumaini una enjoy maongezi haya na Kaka mkubwa na pia confidence yake kwenye masala mbalimbali itakufanya pia ujibebe kuelekea mbele!

Tafadhali enjoy.

Love,
Salama

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Jan 21 2021

1hr 10mins

Play

Ep. 49 - Salama Na MAVOKO | WINGMAN

Podcast cover
Read more

Kwa muda mrefu nimekua nikitaka kuongea na Mavoko ila ratiba zetu zilikua hazijawahi kuwa sawa na hivyo tukawa tunapishana tu. Kama mimi sina program naye basi yeye atakua free, na mimi nikiwa free basi yeye atakua na mipango ya kutoa kazi mpya ambayo itanifanya ningoje ili viende pamoja, au atakua kasafiri, au mimi nitakua nishaset watu wengine, ilikua kama tunacheza kidali po ila katikati ya mwezi wa kumi na mbili hatimaye yakatimia.

Hakuna doubt juu ya uwezo wake popote pale utakapoenda ingawa baada ya yeye kuamua kuondoka kwenye label ya WCB kulikua na mengi yalosemwa na kutendwa na baadhi ya mashabiki yalikua yanaweza kukuaminisha jambo na mpaka kufikia pengine ku doubt huo uwezo wake. Mambo mengi yalisemwa, ya kusikitisha, ndoa haikuvunjika vizuri ila ambacho nilikiona kwake ni ustaarabu wa hali ya juu, wa kuwaacha walimwengu waseme na kufanya watakayo huku yeye akiwa ame focus kwenye kipaji chake na kujipanga upya.

Moto wa Mama Richard anaujua mziki mwingi, ana uwezo mkubwa wa kuimba na kuandika na kucheza pia, ila kabla hajaingia kwenye label alikua anajulikana tu, ila kumfahamu vizuri na kuthamini kipaji chake kulikuja baada ya yeye kushirikiana na mmoja kama si msanii bora zaidi kuwahi kutokea na kuipeperusha zaidi bendera ya Tanzania ndani ya Diamond Platnumz. Ushirikiano wao ulitupa ‘anthem’ kadhaa ambazo mpaka leo ukiziskiliza hazichuji. Ilikua kama team ya wenye vipaji pekee, kama ni mfuatiliaji wa mpira wa kikapu hii tunaweza kuifananisha na ile zile team mbili za Mashariki na Magharibi ambazo zinakusanya wachezaji wenye uwezo wahali ya juu.

Saasa, ikawaje hasa mpaka akaona aachane na all star hiyo na kupeleka team yake uwanjani akiwa solo? Nini hasa kilifanya mpaka afikie maamuzi hayo? Kuna mtu  au kitu kilimshinikiza? Je yalikua maamuzi sahihi? Pia kuna masuala binafsi ya kifamilia na suala la yeye kutomfahamu Baba yake takati anakua, elimu yeke, ndugu zake, Mama yake na muziki ulichomfanyia katika maisha yake.

Mavoko huyu ambaye mimi namfahamu nilikutana naye Kampala, Uganda kama maka saba iliyopita na mazungumzo yetu yalikua yanahusu kipaji chake na jinsi ambavyo nilikua naona ‘hapewi’ nafasi maana kama ngoma zake zilikua nzuri tu, video ndo usiseme ila hakuna na spotlight aliyokua anastahili, peleka mbele miaka mpaka 2021 ambapo alipata nafasi kwa miaka takriban miwili na nusu kufanya kazi na lebo bora zaidi ila baada ya muda akaamua kubwaga? Kwanini hasa? Sote tunajua kama nyasi za jirani huonekana zimestawi kweli kweli ila ukifika na kuziona kwa ukaribu utaelewa kwamba si kila kitu kina fanana na kionekanavyo.  Ila mpaka kuamua kukusanya na mabegi na kuondoka kwenye ‘jumba kali’?

Majubu yake yalikua ya moja kwa moja tu na nafsi yake ilikua tayari kuhamia nyumba nyengine mwenzangu. Natumai kwa kiasi flani utasoma jambo, ingawa kwangu mimi natamani ningepata zaidi na zaidi ila inaonekana bado hakua tayari kutufungukia mazima. Binafsi namshkuru kwa kuja mezani kwetu na pengine tutaweza kukutana tena mbeleni In Shaa Allah. Yangu matumaini bado utaokota mawili matatu.

Love,

Salama.

---

Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Jan 14 2021

1hr 5mins

Play

Ep. 48 - Salama Na JK | MSOGA UNO

Podcast cover
Read more

Muda si mrefu iliopita nilirudi nyuma kidogo kwenye kumbukumbu ya mawasiliano ya kwanza kabisa kati yangu na moja wa wasaidizi wake Mheshimiwa Jakaya Mrisho wa Kikwete na hiyo ilinirudisha nyuma mpaka mwezi wa tatu mwaka 2020. Kama mtu mwengine yoyote hii ilikua ndoto tu ambayo kwa Rehema na Baraka za Allah ilibidi itimie. Kwa Baraka zake hizo mimi na wenzangu tunashkuru sana sana kwa kuweza kulikamilisha hili.

Shukran za dhati ziende kwa Doris Mollel ambaye kwa msaada wa Sadam ‘Almando’ Sanare alinimbia Doris anaweza akatu unganisha na mmoja wa wasaidizi wake ili tuweze kuona kama tunaweza pata hii nafasi, na kama ujuavyo, mengine yote yamebaki kuwa historia tu tena, maana yametimia.

Mimi kama wewe tu, shabiki nambari moja wa Jakaya Mrisho Kikwete na kukutana naye, kukaa naye chini na kuweza kumuuliza maswali tuliyokua tumeyaandaa (kwa muongozo wao) ilikua raha isiyoelezeka. Mzee charming, mwenye roho nzuri na muelewa kabisa. Mengine yalofuata baada ya hapo ndo ambayo utayaona au kuyaskiliza katika maongezi yetu haya. Mengi yalikua ni juu ya yeye alivyokua na uelewa wake kwenye mambo mengi. I wish tungeweza kuongea nae kuhusu masuala meeengi zaidi kuhusu kiila kitu ila ki ukweli hii inatosha kwa sasa na Mungu atajaalia tutakutana naye tena siku nyengine In Shaa Allah.

Mheshimiwa JK aliongea nasi kuhusu Wazazi wake, elimu, uelewa wake wa mambo, yeye kuwa mwanajeshi. Jinsi alivyokutana na Mama Salma. Historia ya nyuma kidogo kuhusu mapenzi na jinsi Marehemu Mzee wake alivyomtaftia mke na kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza ambaye ni Ridhwan. Kuhusu kitabu chake, mapenzi yake na basketball na muziki. Pia Kobe Bryant na mapenzi kwa wajukuu zake.

Kama ilivyo kawaida yetu, yangu matumaini utapata kadhaa humu ya kukufunza jambo. Na napenda kuchukua nafasi hii kumshkuru kila mtu ambaye alisaidia hilo kutimia na zaidi team yangu yote ya ‘YahStoneTown’ ambayo ilifanya kazi iliyotukuka kukamilisha hili.

Nikutakie Kheri ya mwaka mpya na kila lenye Kheri nawe.
Enjoy.

Love,
Salama.

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Jan 07 2021

1hr 1min

Play

Ep. 47 - Salama Na JOTI | SIMPLY SPECIAL

Podcast cover
Read more

Lucas Mhaville ni maalum sana, kwa ki vyovyote vile utakakavyotaka wewe, ki maisha, ki muonekano, ki uelewa na jinsi anavyokua mpya kila siku kwenye ulimwengu wake, jinsi anavyo jipa matawi na kujigawa kisanaa. Jinsi anavyotoa character wapya kila mara kwaajili tu ya kuleta ladha mpya kwenye sanaa yake, hili linamfanya aendelee kuwa mchekeshaji pekee kwenye kizazi chetu ambaye huwezi kuona amechuja au hana jipya kwenye kukufurahisha wewe.

Kabla sijaiandika hii, kipande kidogo cha video kilienda kwenye ukurasa wangu wa Instagram (@ecejay) kwaajili ya kuwafahamisha watu kwamba JOTI atakua ndo mgeni wetu wa usiku wa leo, na kwenye hiyo video nilimuuliza kuhusu kabila lake ambalo kwa mujibu wake ni kabila dogo tu kutoka huko Morogoro na yeye na Baba yake mdogo ambaye ni Polisi ndo watu waarufu zaidi, ila kwa wingi wa replies kutoka kwa watu wengi wa kabila hilo inaonyesha si kabila dogo kama yeye alivyodhani, ila hiyo ni tisa, kumi ni jinsi ambayo watu WANAMPENDA na kusikiliza KILA ANACHOSEMA, hiko ni kipawa tofauti kabisa, sio kila mtu anaweza kuwa na uwezo huo.

Yeye ni mzaliwa wa Morogoro na alikuja Dar es Salaam baada ya mzazi wake mmoja kufariki, alichukuliwa na ndugu yake na kuja kulelewa hapa, amesoma hapa na sanaa yake pia ilianzia hapa alipokua shuleni. Nani alimsukuma? Na je alisoma mpaka daraja lipi? Mimi na yeye pia tunazungumzia umuhimu wa elimu na malezi bora. Maisha yake alipokua mdogo na mafunzo aliyoyapata growing up.

Joti si wa leo, akiwa na miaka yake 38 anajielewa vizuri sana tu. Maongezi yetu pia yalitupeleka kwa uanzishwaji wa kundi la Original Comedy ambalo lilitufanya sote tuwapende sana na enzi hizo za EATV wao wanapokua hewani basi nchi nzima ilikua inasimama kwaajili ya kuangalia walichotuandalia. Yalikua mafanikio haswa! So nini kilitokea mpaka wakaomdoka EATV? Na wao kama kundi kuna lolote kwa sasa? Au kila mtu ndo solo? Na vipi kuhusu Vengu? Yule mwenzao (mwenzetu) ambaye alipata matatizo makubwa ya ki afya na mpaka naandika hii bado yuko kitandani? Shida yake hasa ni nini? Haina tiba?

Humu pia tumeongelea mahusiano yake na Seki, ambaye alikua naye toka enzi za OC akiwa kama kiongozi na mtayarishaji. Mahusiano yake na Mpoki, Masanja ambaye sasa amejikita kwenye masuala ya ki kanisa, Wa Kuvanga na McRegan? Wako wapi? Kama kuna comeback ya kundi? Lini?

Wakati nafanya hii pia nilitiwa elimu na Director wangu wa siku hiyo (Ms Lydia Igarabuza) kwamba, ukitaka kuongea na mchekeshaji, ili upate utakacho, basi usimpe nafasi ya yeye kukuchekesha mpaka ukasahau kilichomleta pale, namshkuru sana kwa hilo maana nadhani ki kawaida kama wana tungecheka zaidi kabla ya kuyasikia yote ambayo tumeongea humu.
Respect nyingi ziende kwa Joti ambaye ameweza ku maintain status yake ya heshima ya juu kwenye kazi yake, na kama binadamu.

Yangu matumaini utaokota mawili matatu hapa ambayo yatazidi kukutia mafuta ya kukufanya utake maendeleo zaidi na heshima kwenye jina lako na maisha yako.
Tafadhali enjoy.

Love,
Salama

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Dec 24 2020

1hr 19mins

Play

Ep. 46 - Salama Na HK | NJE YA BOX KIDDOGO

Podcast cover
Read more

Sikuwahi kuujua ufahamu wa Dr Hamisi Kingwangala kwenye suala la dini kwa kiasi ambacho ameniambia wakati tunaongea kwenye kikao chetu hiki, na alinilelezea kwa majina yake ya kizuoni huku akiniambia nini kwa binafsi yake anaweza kukifanya kwa kituo pale anapotaka, lakini pia aliniambia juu ya suala la yeye kutokua anaswali sala tano kama ilivyokua zamani na kwamba si jambo analojivunia asilan!

Hii ilikua mara yangu ya pili kukutana na kuongea nae kwa kituo, kama ilivyokua kwa Taji nae pia niliongea naye miaka ya nyuma wakati nafanya Mkasi, na kwa kuongea naye round hii nimejifunza kwamba hawa ni kama watu wawili tofauti kabisa na si kwa ubaya, yule wa kwanza alikua si muongeaji kama huyo wa sasa  kwasababu amekua kwa kiasi flani na kukua ni jambo ambalo sisi wenyewe na wazazi wetu huangalia kwa makini kuanzia pale ulipokua tuseme miaka mitano iliyopita na sasa na mipango na maratajio yako. Kwa hili Sheikh HK kaserebuka nalo vizuri tu. Hakuna mtu asiyemfahamu Hamis Kingwangala ndani ya nchi hii na nje, jinsi ambavyo alifanya kazi nzuri ya kampeni ya kuitangaza Tanzania duniani kwa umaarufu wa vivutio vya utalii wetu na utajiri wa nchi yetu pendwa. Alichukua muda huo pia kutembelea karibu mbuga zote na nchi hii na wakati huo huo kupambana na majangili na waharibifu wa wanyama pori, vita ambayo ilikua ndo stori ya kipindi flani hapo nyuma. Yeye HK alikua anamalizana na maneno ya walimwengu ambao walikua wanaongea mengi kwenye mitandano ni kwa  yeye. kuendelea kupiga  kazi yake vizuri tu mpaka akamaliza miaka mitano ya kwanza ya Rais aliyempa cheo hicho kwa usalama tu, nasema hivyo kwasababu kuna wengi ambao walikua wanateuliwa lakini siku zao za kukaa ofisini hazikua nyingi sana ila HK aliweza kuendana vizuri na mawimbi kwenye bahari ya uongozi ambayo bila ya shaka ilikua na mitihani yake.

Pia umaarufu wake mwengine Bwana HK ulikuja baada ya kuwa ntumiaji mzuri sana wa Twitter, sehemu ambayo huitumia kwa kufanyia kazi yake ya kuitangaza nchi na pia kumalizana na ‘wabaya’ wake wote ambao wamekua wakila nae sahani moja kila mara panapokua na jambo ambalo yeye amesema au kuwakilisha mooni yake juu ya suala flani. HK hana tabia ya kuona haya kumjibu mtu ambaye kwa namna moja ama nyengine anakua kamgusa pale alipokua hapataki yeye au pengine tofauti tu ya mawazo, muda mwengine utakuta watu wamefika huko.

Kubwa kuliko ilikua hii ya mwaka huu ambayo alihoji juu ya uteuzi wa CEO mpya wa klabu yake pendwa ya Simba na pia suala la mwekezaji kutimiza ahadi yake ya kuipa Simba shilingi bilioni 20 za kuendeleza klabu. Hili suala liliamsha zogo kubwa kati ya HK, muekezaji wa klabu pamoja na mashabiki wa Simba, lilifanya pia tujue siri za ndani za kibiashara kati ya wawili hawa na jinsi ambayo wote wawili walivyokua wanajibizana mitandano ilifanya watu wengi wanyanyue nyusi kwa mshangao na kujuzwa mambo ambayo pengine yalikua hayana faida kwa watu wengine kujua. Hivi karibuni wawili hawa walimaliza tofauti zao huko huko kwenye mitandao hiyo hiyo ya kijamii kama walivyofanya awali.

Niloitaka kujua kama kuna muendelezo wa hayo maongezi yao, kama walishakutana toka majibizano yale yatokee, pia tuliongelea ajali ambayo aliipata akiwa kazini na ambayo pia ilizungumziwa na watu wengi. Pia niliongea nae kuhusu Rais Magufuli, uchaguzi wa mwaka huu ambao chama chake kimeshinda  kwa ushindi mnono na jinsi ambavyo hakupata nafasi kwenye baraza la mawaziri na manaibu wake ambalo limeundwa hivi karibuni na ambavyo aliipokea taarifa hiyo.

HK ni mtu poa sana, kijana ambaye ni Kiongozi, Baba, Kaka na mfanyabiasha mzuri tu ndo darasa letu la wiki hii na yangu matumaini kana kawaida atakua na jambo la kukufunza kwahiyo tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

---

Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Dec 17 2020

1hr 34mins

Play

Ep. 45 - Salama Na TAJI | TABASAMU LA SWAHIBA

Podcast cover
Read more

Pia anafahamkika kama Master T, mwenye sauti yake tamu ya kumfanya mtu abadilishe mawazo na kufanya anachosema yeye, lafdhi nzuri ya maneno ya Kiswahili na Kiingereza na tabasamu zuri kabisa lililokaa mahala pake na hiyo ndo tofauti ya Taji Liundi na watangazaji pamoja na hata viongozi wa department mbali mbali kwenye vyombo vyetu vya habari vya ‘siku hizi’.

Taji alibahatika kuzaliwa kwenye familia yenye uwezo kwa kiasi chake na malezi bora aliyapata kwa Baba yake ambaye muda mwingi alikua akisafiri nchi mbalimbali kutokana na kazi yake na hii pia ilimfanya ajengeke kwa kiasi flani, kuweza kujiamini, kuongea lunga zaidi ya moja na mapenzi yake na muziki pia yalianzia hapo. Aliniambia katika maongezi yetu haya kwamba kukaa na Marehemu Mzee wake ambaye alikua busy wakati mwingi ndo ulimpa mwanya wa yeye kujifunza mambo mengi ya nje ikiwa ni pamoja na muziki na michezo kama football na basketball. Pia aliniambia alikua mpigaji simu kwenye radio mzuri sana tu, na kwa kiasi flani hiyo ilifanya mapenzi yake na radio yaanzie na aliporudi nyumbani na familia yake alipata msukumo wa kwenda kutafuta kazi kwenye radio.

Kuna tukio pia lilitokea vacati akiwa na umri kama miaka saba au nane ivi, ambalo lilikua linahusiana na wivu wa mapenzi ambao Mama yake alikua nao kwa marehemu Mzee wake na ndo ambalo lilifanya maisha ya Taji yabadilike sana sana. Na hihi simulizi alitupa kwenye kipindi chetu hiki, hii ni tettes ambayo niliiskia mara nyingi tu wakati nakua na kistaarabu kabisa ilibidi nimuulize Kaka yangu kama atakua huru tuizungumzie hapa, na hakua na hiyana kabisa. Tuliongelea jinsi ambavyo Mama yake aliwauwa ndugu zake na jinsi ambavyo yeye aliponea chupuchupum anatuelezea vizuri sana kwenye maogezi yetu haya.

Taji pia alikua boss vanga wa kwanza mimi kama Salama, kazi yangu ya kwanza yeye ndo alinipatia nafasi kwa moyo mmoja kabisa, aliniambia nifanye majaribio ya sauti na kusoma habari flani ya Tennis na mengine baada ya hapo ni history kama wazungu wanavyosema. Kwahiyo pia nilimuuliza kiaina ni nini hasa aliona ndani yangu na kama anaikumbuka hiyo siku, maana binafsi nakumbuka mpaka nilichokua nimekivaa Salama mimi. Maneno pekoe hayawezi kusimulia jinsi ninavyo mshukuru kwa kuniamini na nafasi, Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda, kumpa afya njema na kumtimizia kila takwa la moyo wake In Shaa Alla.

Kwa kumalizia pia mi Kaka yangu tulizungumzia mustakabali wa muziki wetu na  wanamuziki wetu, radio na watangazaji wa kisasa na pia muongozo kwenye masuala ya kazi, Taji pia aliniambia naye ameanza kutimiza ndoto zake kidogo kidogo kwa kutoa single yake ambayo hata mimi nilishtuka kidogo kwa furaha baada ya kuona yuko serious, na sio wimbo tu, ni wimbo MZURI.

Nilienjoy sana kuongea na Taji kwenye kipindi hiki na zaidi nilifurahi kwasababu anakua anapatikana pale unapomhitaj, hii inakuja hata kwako wewe, kama utakua unahitaji ushauri wa masuala ya kazi na hata maisha, Taji hatokosa la kukuambia ambalo litakufanya ujiskie vizuri, na kuzogeza mambo, hilo nakuahidi.
Hii nimeifanya kwaajili yangu na yako na yangu matumaini itakufunza jambo na kukufanya utabasamu.

Love,
Salama.

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Dec 11 2020

49mins

Play

Ep. 44 - Salama Na MWAKINYO | VITASA OVERLOAD

Podcast cover
Read more

Hassan Mwakinyo kwa Mama yake ni kama ni kama mkate kwa chai tu, lazima ulainike. Sentensi hii imeanzia hapa baada ya kufuatilia kwa makini na kuambiwa hasa ni kitu gani kinachomfanya Champez atake kuwa bora zaidi na zaidi, na kutaka kupata kile anachokipata kwa nguvu zaidi na zaidi kila siku kila asubuhi anapoenda kukimbia, au kila jioni anapokua gym au anapokua ulingoni, na amini kwamba Mama yake ndo anayemfanya atake kuwa bora siku zote ili aweze kumbadilishia maisha yake kwa uzuri.

Champez Mwakinyo sio moto pekee kwenye familia yao na Kaka yake mkubwa alianza haya mambo ya ngumi kwanza kwa kujiingiza kwenye kick boxing na akawa sio mkali au hodari vile kama ambavyo Mwakinyo amefikia lakini muongozo wake ndo ulomfanya Champez awe hodari kiasi hiki na kuna mpinzani ambale alikua anamsumbua sana kaka yake ila baada ya miaka kadhaa Mwakinyo alimalizana naye vizuri tu na kuweka heshima kwenye familia.

So niliongea na Mwakinyo kuhusu ile fight ambayo ilitufanya sote tumfahamu uzuri, nilitaka kujua alifikaje kule Liverpool na yule mpinzani alimpataje? Vipi na yule jamaa ambaye alibeba headlines zaidi kuliko hata Mwakinyo mwenyewe? Walikutana vipi? Ni kweli alikua anamtaka Kelly Brook? Au yeye mkalimani ndo alikua na ajenda hiyo? Je kuna siku tutaweza kuiona hiyo fight?

Mambo mengi yalitokea wakati Mwakinyo akiwa Uingereza, kulikua na suala la kuchukua pesa na kuacha apigwe kulikua na suala la yeye kupotea kabla ya kwenda kupima uzito. Suala la Mama yeke kupata ajali kabla ya yeye hajaenda England na mambo mengine kibao. Alirudi pia nchini na akapata kudhaminiwa na kampuni moja kubwa ya masuala ya betting, huo mkataba uliishaje? Alipata faida yoyote?

Hivi karibuni alipigana na Jose Carlos Paz kutoka Argentina ili kuweza kutetea ubingwa wake wa WBF kutoka IBA hapa jijini Dar es Salaam, pambano lilikua la kiwangi cha juu, la kimataifa tuseme lila kwenye suala zima la uandaaji na viingilio kama lilileta utata kwa mashabiki zake. Nilimuuliza Mwakinyo kama kile ndo alichokua anataka maana kwa uelewa wangu, boxing ni mchezo wa watu wa chini hapa nyumbani kwetu, je ilikua sawa kwa yeye kukubali viingilio vile? Au inabidi tukubaliane kwamba enzi zimebadilika na kwamba mambo ndo yaka hivyo now?

Nini kinafuata kwake? Nini anataka kwenye maisha yake? Vipi kuhusu mpinzani wa hapa nyumbani ambaye wapenda ngumi wengi ndo wamngependa apigane naye? Maoni yake yepi? Kweli tutaweza kuona hilo pambano? Tulitegemee lini? Jibu lake ndo litakupa muongozo kama tunayoyataka yatakua au la!

Yangu matumaini Champez atakufundisha mambo kadhaa kuhusu heshima, mapenzi, malengo, dini na kujiheshimu na jengine lolote ambalo unaweza ukapata humu. Tafadhali enjoy.

Love,
Salama.

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Dec 03 2020

1hr 2mins

Play

Ep. 43 - Salama Na MANTANA | MIPANGO BAABA

Podcast cover
Read more

Sniper Mantana si jina lake la Serikali na ukiskiliza kwa makini kwenye maongezi yetu haya utaelewa uzuri kwamba jina hilo alipewa kutokana na umahiri wake wa kulenga pale kwenye malengo yake na kufanikiwa kutokana na juhudi zake ambazo unaziona hata kwa mbali tu na ki ukweli kabisa hiyo ni moja ya sababu kubwa ilonifanya nitake kukaa naye chini ili anifahamishe hasa siri ya mafanikio yake na kile kinachomsukuma kufanya afanyayo.

Mara ya kwanza kumsikia Sniper ilikua kutoka kwa AY ambae yeye walikutana huko Malaysia na alikua ni msanii wa kwanza kwenda kutoa burudani huko, Sniper ndo alifanya mipango yote hiyo. Alikua na uwezo wa kuwakusanya wanafunzi wenzake wa ki Tanzania, Kenya na Afrika kwa ujumla na hata wageni wa mziki wetu pamoja na kuwapa burudani kutoka ukanda huu. Alifanikiwa, aliweza kuwa na sehemu ya kupiga disco na concerts na aliweza kusoma na kurudi na digrii yake vizuri tu kabisa.

Kampuni yake ya Straight Up Vibes ndo kinara sasa hapa kwetu kwa kufanya kazi nyingi za makampuni na promotion ila pia yeye kama yeye pia ni promoter aliyetulia kabisa, anayejielewa na ambeye pia amefanikiwa vizuri kuliteka soko la muziki hapa nyumbani kwa kuweza kuwaleta wasanii wa nje ambao wameweza vizuri tu kwa kutoa burudani ambayo wanastahili kwa viingilio vikubwa wanavyolipa.

Kampuni yake ilifunga mwaka jana kwa concert ya heshima kabisa na mwaka huu ameuanza vizuri tu kwa kuendeleza pale alipoishia.

Humu, binafsi nilitaka kujua safari yeke na mambo mengine kama haya lakini pia niliongea nae kuhusu mustakabali wa muziki wetu hapa nyumbani, kwa kirefu tu. Yeye kama promoter amekua akidondosha wasanii wengi hapa ambao wengi wao wamekua wakilipwa mapene mengi na hilo likasababisha baadhi ya wasanii na raia wa kawaida kuuliza maswali juu ya sisi kuendelea kuwatajirisha wenzetu wakati hapa nyumbani yuna vipaji vikubwa ambavyo navyo vilikua vinahitaji kupewa mapene hayo , na kama kuna sehemu wanakosea basi waambiwe ni wapi ili nao watoke! Mantana hakua mchoyo juu ya nini kinatakiwa kufanywa na pia kwamba mlango wake uno wazi kwa yoyote atakayehitaji msaada wa jinsi ya kufanya mambo kadhaa ili vitu viende.

Sniper ni MTANZANIA, kijana aliyeenda shule na kumaliza kabisa na kupata cheti chake freshi kabisa. Hakukimbia DARASA, alifanya alichokifanya na kujifunza along the way, elimu ambayo inamfanya atoe ajira hapa nyumbani na kuishi vizuri pia. Nilimleta hapa ili yatu waskie alipotoka na nia na madhumuni yake huko mbeleni na kama vipi uchote mawili matatu ili yaweze kukusaidia hapa na pale. Tafadhali Enjoy.

Love,

Salama.

---

Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Nov 26 2020

1hr 37mins

Play

Ep. 42 - Salama Na EDO KUMWEMBE | MWENYE SHOKA HAKOSI KUNI

Podcast cover
Read more

Edward ‘Edo’ Kumwembe ni rafiki yangu wa si miaka mingi, pengine sita tu toka mara ya kwanza kukutana nae wakati wa uzinduzi wa kampuni moja ya kamari hapa nyumbani. Nakumbuka alikua akimtania sana Fid Q na jinsi ambavyo Fid alikua hamjibu Edo ndo ilikua inachekesha kabisa, wengi wetu tunafahamu Fid ana maneno mengi, ila mbele ya Edo huwa hana hata maneno kabisa. Tulicheka sana, na baada ya hapo tukaanza kufanya kazi pamoja kama Influencers kwenye hiyo kampuni, na baada ya miaka  mitatu Allah akabariki nikapata ile kazi ya Super Sport, na kama ulikua hufahamu, Edo ndo alinipigia chepuo nyingi sana ili niweze kuipata hiyo kazi ambayo kiiila ‘mchambuzi’ wa futiboli alikua anaitaka, mpaka baadhi ya wastaafu na viongozi walikua wanaitolea macho, lakini Mungu akanibariki nayo mimi Salama. Yeye pia (hii ilikua siri 😃) ndo alikua mtu wa kwanza kuniambia kama mkeka umetiki, tunaenda zetu Johannesburg. Furaha yangu ilikua kubwa sana, na nilikua napiga kelele ndani yangu, ila kwa nje nilikua na play cool, najifanya oh. okay…Habari nzuri hii Edo, asante sana. Kumbe ndani kuna Meja Kunta anaimba singeli kwenye pati ya kitaa, kelele nyingi sana.

Mungu si Athumani na safari yangu kwa kwanza ya KIKAZI ilikua ya AFCON2018, unaweza aka guess ni nani nilipangiwa kufanya nae kazi kwenye kuanzia mechi za mtoano mpaka fainali hizo? Ndio umepatia, ni Edo Kumwembe. Alifanya maisha yangu yawe rahisi sana. Alinisaidia sana kunitoa hofu na kunifanya niwe calm na kuweza kuifanya kazi ile kwa uzuri kadri ya uwezo wangu, akiniona tu niko down au siko 100 alikua akiniambia, ‘oya, hii kama ubwabwa tu’. Huo ulikua ni msemo wa Maulid Kitenge ambao Edo aliuleta kwangu akimaanisha hii kazi ni rahisi sana, ni kama kula wali tu 😄. Mungu ni mwema. kazi ilienda freshi, Edo alinipa bata la kufa mtu. alinionyesha (na bado anaendelea) kunionyesha Jozi. Ananifundisha mambo mengi kuhusu soka na watu wake na kila kitu chake kila siku, hata kama haniambii mimi ila najifunza tu kutoka kiwale kila siku.

So nini hasa ambacho kinamfanya Edo awe ‘mnyama’ kiasi hiki? Well, ndo Mungu alivyo mbariki. Hana kununa wala kulalamika ili mambo yawe magumu, yeye huchukulia vitu kwa wepesi tu na kumalizana navyo vizuri tu. Anafanya anachokitaka kwa wakati wake. Hana majungu, hasemi pembeni yani, kama ana la kukuambia basi jua atafanya hivyo bila ya kukupepesa, kitabia flani ambacho tunafanana kiasi. Urafiki wetu pia unaendana kwa kupenda kucheka, kama nilivyosema awali, ukikaa naye kucheka ni uhakika na hilo pia ni jambo langu pendwa kabisa. Inawezekana ikawa anakusema wewe mwenyewe mpaka inabidi ucheke tu, inawezekana ikawa kuhusu football, au siasa au muziki au maisha, mapenzi yani wewe tu. Kusema za ukweli ni raha tu ukiwa nae. Pia anapenda MAISHA MAZURI na haogopi kuyafanyia kazi ili aishi hivyo. Pia yeye ni moja wa waandishi wa habari wachache sana ambao wanajituma sana, Edo anaweza kuweka hela zake akasafiri tu ili aweze kufanya interview zake na zikawa tofauti kabisa na waandishi wengine. Hii inampa uwanja wa kufanya vizuri zaidi na kupa uhuru wa kuongea anachokijua na sio kuongea tu kutokana na alichosoma kwenye internet.

Tulipokutana mezani tuliongea kuhusu yeye kama toto kutoka kwenye familia ambayo haikua vibaya, familia ya kisomi tunaweza kusema. Vipi alianza kufanya anachofanya sasa? Nani alimvutia? Pia kuna mustakabali wa mpira wetu hapa? Simba na Yanga? Ni kweli soka letu limepanda kiwango? Vipi kuhusu wachezaji wetu wanaocheza soka nje ya Tanzania? Chama cha mpira je? Viongozi wake? Mpango wa mbeleni anauonaje? Je, unafahamu kama Edo pia ni muandishi mzuri sana wa makala mbalimbali kwenye gazete la Mwananchi na Mwanaspoti?

Maongezi haya yangeweza hata kufika siku ya pili maana mimi na yeye tunaweza kuongea na kucheka  for days ndo maana mimi na wenzangu tukaona sio mbaya kukuletea Kaka hapa ili nawe ufaidi na kujifunza kama ambavyo mimi nafanya. Yangu matumaini ata enjoy.

Love,
Salama

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Nov 19 2020

1hr 12mins

Play

Ep. 41 - Salama Na KALITO | THE ORIGINATOR

Podcast cover
Read more

Carlos Bastos aka Kalito ni moja kati ya wale binadamu ambao hawahitaji ‘kutambulishwa’ na hiyo si kwa sababu ya muonekano wake hata kidogo zaidi ni personality yake, anaongea, anachekesha, anajielewa, anajua nini cha kusema na wapi pa kusema pia. Katika watu ambao namshukuru Mungu kwa kuwafanya wawe rafiki zangu Kalito ni mmoja wapo.

Jinsi ambavyo alifika Tanzania inaweza ikakufanya ujue pia yeye ni mtu wa aina gani haswa, kutoka mwenyewe familia ambayo mtoto wa kiume ni pekee, na pengine alikua na uhakika wa kupata kila anachotaka lakini aliamua kupaki begi na kuchanja mbuga kuja hapa Tanzania. Kusema za ukweli story yake ya maisha ni ya kuamsha sana. Imagine wewe leo unatoka ulikotoka ukaenda zako pa kwenda, ukajimix kwa kuhudumia watu kwa kuwapa burudani na chakula mpaka akapata upenyo wa kufanya yake. Ni wangapi kati yetu wanaweza kufanya hivyo? Najua wengi wetu hatukuzaliwa hapa Dar es Salaam ila tumekuja tukalikita na mpaka sasa Alhamdulillah mambo yanaenda. Ila si wengi wanaweza kusema hivyo. Tunajua huchukua jasho machozi na pengine damu kufikia malengo.

So binafsi haswa nimejifunza au najifunza nini kutoka kwa rafiki yangu huyu kila siku? Cha kwanza ni kuwa MKWELI. Kama unayo unayo, kama unaweza kufanya/kufika utafanya hivyo, kama unaweza kutoa unatoa na kama huwezi UNASEMA. Naamini ndani ya moyo wangu, hiyo ni moja ya silaha kubwa sana kama unataka kufanikiwa, kama unataka MAENDELEO. Cha pili pia ambacho bado kinakaa kwenye UKWELI ni UAMINIFU. Ukikopa pesa RUDISHA maana hii itakupa nafasi ya kuweza kurudi na kukopa tena kama mambo yako yatakua bado sio sukari, sasa imagine hujarudisha na ukapata shida nyengine je utaweza kurudi kukopa tena? Vipi kama alokukopesha nae kashawaambia ma don wenzake kwamba wewe huwa hulipi? Utasogea kweli?... Mwisho wa siku DAWA YA DENI ni KULIPA tu.

Jengine KUBWA zaidi ni kutokua na SIRI nyiiiingi. Mambo ambayo yatakufanya uwe unaweka vitu vingi ndani, ambavyo hauwezi kusema labda kwasababu ya aibu au pengine hauko huru kuviongea nalo ni TATIZO. Ni kweli sote tuna SIRI zetu, ila zikizidi ndo zinaleta msongo wa mawazo. So kuwa muangalifu na kipi unasema na kipi unaweka. Kujijazia mavitu moyoni ki afya si mpango hata kidogo.

Kalito yuko HURU, anaskiliza watu na kujifunza kila siku pia kama mimi na wewe tu, pia ana shida zake ambazo kwa kiasi kikubwa ameweza kuzifanya zisiwe chanzo cha yeye kutokua na furaha au kumpa unyonge. Pengine unaweza kusema ni kwa sababu ana hela au biashara inayomuingizia kipato kila siku ndo maana ni rahisi kwake kucheka kwa yote, ila Amini nikikuambia hata yeye huwa ana kutana na mitihani mikubwa tu, lakini kwasababu yuko POSITIVE muda wote unakuta anamalizana na shida zake kwa roho safi tu. Anakubali pale anapokua kashindwa na kujifunza na anafurahia pia challenges ambazo binafsi anazishinda kwa uzuri tu. Yeye pia ni rafiki nambari MOJA wa wafanyakazi wake karibia WOTE wa Samaki Samaki na sasa Kuku Kuku wa kuwajua mmoja mmoja kwa majina yao. Mpaka mafundi wake wote hao ni familia yake.

Wangu tumekuletea Kalito kwenye meza ili uone mambo kwa utofauti haswa. Ujifunze kutoka kwa watu ambao unawaangalia kila siku na ambao pengine unadhani mambo yao ni SUKARI kila siku iendayo kwa Mungu. Yangu matumaini utaokota mawili matatu humu. Maana ukiachana na biashara pia alizungumza maisha yake. Alivyoumwa, watoto wake na jinsi alivyofika Tanzania na nchi yetu hii na watu wake. Alituambia pia kuhusu mapenzi yake na Bahari na mahusiano yake na watoto wake na Mama yao ambaye hayuko nae tena sasa. Tafadhali enjoy.

Love,
Salama.

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Nov 12 2020

1hr 19mins

Play

Ep. 40 - Salama Na KADUGUDA | SIMBA WA YUDA

Podcast cover
Read more

Mara ya kwanza kukutana na Mwina Kaduguda na tukaongea kiasi ilikua kwenye seminar ambayo timu ya Simba ya wanawake ilikua imeandaliwa kwaajili ya kuwaweka sawa kwenye masuala ya biashara, jinsi ya kujitunza wao na vipaji vyao, jinsi ya kuishi na umaarufu na pia kusimamia masuala yao ya kifedha. Mzee Kaduguda alikuwepo kwenye kikao hiko akiwa kama Mwenyekiti wa klabu ya Simba, na pia mmoja wa watoa nasaha kwa mabinti hao.

Na kusema za ukweli toka siku hiyo baada ya kumsikiliza akiongea na wachezaji wale pamoja na Mimi ambaye nilikua mgeni tu kwenye seminar ile, nilivutiwa sana na nikasema haitakua vibaya hata kidogo kama nikipata wasaa wa kuzungumza na mtaalam huyu wa Siasa za kambumbu la Tanzania na Afrika kwa ujumla, mwamba ulojaa uerevu wa kusoma kuhusu soka letu lakini zaidi historia ya Simba Sports Club na zahma za hapa na pale pamoja na siku za neema zaidi ambazo zimeshawahi kutokea pale Msimbazi, mtu pekee anayeweza kukukhadithia yote hayo ni Mwina Mohamed Seif Kaduguda.

Toka siku ya kwanza alipomuambia Mama yake mzazi ndoto zake na ambae pia alicheka sana, Mwina hakuwahi kurudi nyuma asilan, badala yake alisoma kwa bidii mno mpaka siku alipofika chuo kikuu. Na baada ya hapo pia hakuacha kujiendeleza, aliendelea kwa kusomea leseni kwa kufundisha mpira na hapo ni baada ya kuwa mmoja wa waandishi wa habari za michezo waliobobea kabisa. Alitaka kuwa tofauti na bora kuliko waandishi wengine, na alifanikiwa vizuri tu.

Msukumo huo sasa unatoka wapi? Na pale Simba Sports Club aliingiaje? Lini ndo alijua ana mapenzi na club hii na si nyengine? Kuna mtu alikua anamvutia? Alimshawishi? Alishawahi kuichezea? Alishawahi kuwa footballer yeye? Vipi uongozi alifikaje huko? Na ramani ya soka letu je anayo nani? Inasomeka? Kuna kitabu cha historia ya Simba SC toka miaka ya mwanzo kabisa yeye ndo aliandika, je nini kilimpa msukumo? Inasemekana ndo kitabu ambacho kimefanyia research na kuandikwa vizuri zaidi, je kuna ukweli ndani yake? Na kwamba kinauzwa bila ya yeye kupata malipo yoyote?

Akiwa kama Mwenyekii wa SSC yeye haswa jukumu lake ni nini? Kuna ukweli wa hizi habari kuhusu tajiri kutoweka hela alizo ahidi? Yeye kama Kiongozi hili analizungumziaje? Mipango kwenda mbele ikoje? Na vipi kuhusu uhusiano wake na Mo Dewji? Na maamuzi ya kuwa CEO wa klabu ni MWANAMKE hayo vipi? Na je alishirikishwa kwenye maamuzi hayo?

Enjoy mazungumzo yangu haya na Simba, ingawa alikua mzungukaji kweli kwenye ujibuji wa maswali yangu niseme tu nimemuelewa. Hakuna kitu kinajengwa ki rahisi au kwa siku moja. Simba Kama klabu inabidi ipewe muda na mipango thabiti ili kufika kwenye malengo makuu na Ndugu Mwenyekiti hilo analitambua.

Regards,
Salama.

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Nov 05 2020

1hr 15mins

Play

Ep. 39 - Salama Na DULLA | GO HARD OR GO HOME...

Podcast cover
Read more

Abdallah Khamis Ambua ndo jina halisi toka kwa wazazi wake ambao hawana asili ya kisiwani wala kuwahi kuishi huko kwa muda mrefu ambako pengine ndo kukamuwezesha kupata hiyo lafdhi. Kabla hatujafika kokote kwa kuskia kutoka kwangu, ningepeda ufahamu kwamba mimi si mmoja ya watu walotaka Dulla apewe kipindi cha Planet Bongo mwaka 2018 wakati naenda zangu Cardiff kushangaa kondoo, na moja ya sababu zangu kubwa ilikua yeye kutokua na lafdhi nzuri ya maneno kwenye lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Na hilo nililiweka wazi haswa. Lakini pia nilikubaliana na matokeo baada ya viongozi kuamua kumpitisha yeye, na kwa heshima zote leo napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya, kwa kuona kijana ambaye alikua na utayari kwa kujifunza, wa kujua kwamba alikua hajakamilika na mlango ukawa wazi kwake kutaka kujifunza na kuwa bora.

Tupeleke miaka mbele mpaka 2020, ingawa hapo nyuma tushakutana mara kadhaa na nikamuambia jinsi ambavyo ananifurahisha kwa kukuwa kwake na kwamba mimi ni mmoja wa watu wanao jivunia yeye. Na hata wakati tunafanya maongezi yetu haya, nilimfahamisha pia. Mwanzo wakati naanza kuandika nilianza kwa kukuambia kuhusu asili yake, sababu ilikua ni juu ya lafdhi yake ya kimwambao ilonyooka haswa. Mimi wakati nakutana na Dulla kwa mara ya kwanza kwenye usaili hakua na hiyo accent, alikua na matatizo ya R na L na pia hakua ‘original’, alikua ana tangaza na kuongea kama B Dozen, ambaye tayari alikua amesha ji establish vizuri tu na anga yote alikua anaunguruma yeye mara ifikapo saa nane kamili ya mchana. So kama mtangazaji mpya anayechipukia, Dulla hakua na nafasi ya kuweza kutamba mbele ya Dozen, na wala hakua na uwezo wa hata robo yake. Kwa yeye kutoboa na kuweka alama yake ilikua inambidi awe YEYE na aje na ladha YAKE.

Leo hii, mimi na enjoy haswa ninapomsikiliza Mjukuu wa Ambua radioni, sauti tamu, matamshi yamenyooka, ladha ya maneno inatulia maskioni, hapayukwi kwenye kipaza sauti na pia kubwa kuliko yote ana akili, akili ya kusema na kuuliza maswali muafaka na muda muafaka. Na kwa hilo namheshimu.

Basi nikataka kujua vile alijiskia alipong’amua kama mimi sikua shabiki yake hata kidogo? Na Kama ilimtoa katika ‘mchezo?’. Wakati mshindi wa mtangazaji mpya wa Planet Bongo anatangazwa tayari Mimi nilikua nishafika zangu Cardiff kwahiyo sikuwahi kuongea nae tena kuhusu uchaguzi wake na wala maendeleo yake kwahiyo hii imekua mara ya kwanza tuna discuss. Pia nilitaka kujua kuhusu mke wake, watoto, Kaka yake ambaye naye ndo alimfanya kwa kiasi kikubwa achague kazi hii anayofanya sasa. Pia kuhusu mahusiano yake na Diamond Platnumz na Ali Kiba, muziki wa Bongo Flava kwa ujumla. Kazi, mapenzi, ujana, dini na yeye kama binadamu. Haya yalikua maongezi flani ya kikubwa ambayo nimefurahi tuliyafanya mimi na mdogo wangu huyu.

Kama kawaida, yangu matumaini hii pia itakufunza jambo, itakutaka uwe bora na kutokubali kushidwa hata kama ulokua unapenda sana akupe sapoti akawa haamini juu ya uwezo wako, hiyo ndo iwe chachu ya wewe kutaka kufanya vyema zaidi.

Love,
Salama

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Oct 22 2020

1hr 11mins

Play

Ep. 38 - Salama Na CHARLES HILLARY | MZEE WA BUSARA

Podcast cover
Read more

Ilinichukua muda mrefu kuweza kupata nafasi ya kuongea uso kwa macho na Charles Hillary, maana toka enzi za Mkasi nilikua natafuta mwanya wa kuweza kukaa nae chini walau kwa hata nusu saa tu. Sikuwahi kukata tamaa badala yake nilikua kama chui kwenye mawindo yake, na mwisho wa siku kwa uwezo wa Mungu, binti yake Faith, Ivona Kamuntu na Mama kule nyumbani waliniwezesha kushinda mechi hii hatimaye. Mungu anajua tabasamu lilikua la ukubwa wa kiasi gani, na pengine hilo linaweza likawa limefanya niwe excited sana mpaka mengine nikayasahau kuyauliza, au kujua naulizaje, au kushangaa sana? Ushawahi kukutana na mtu alafu ukasahau yote ulotaka kuyasema, au kufanya. Ukabaki tu umeganda kama sanamu? Bado? Basi we ngoja tu.

Simkumbuki Charles Hillary wa Radio Tanzania (RTD), namkumbuka wa Radio One zaidi. Wa taarifa ya habari, wa kipindi cha charanga, wa kutangaza mpira, huyo ndo ambaye alinifanya mimi nipende Radio, nipende kuskiliza mpira na pengine kuutangaza. Sauti yake tamu na lafdhi ilonyooka ilikua inakufanya uone kama unaona haswa anachokiongea. Kipaji cha kipekee kabisa. Kipaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambacho pia kilihitaji kujituma na kujitetea na kujiamini sana. Kutimiza ndoto si suala la kulala na kuamka tu, suala la kukosa usingizi. Suala la kutokwa na jasho, suala la kulia kwasababu tu unadhani hakuna anaye skiliza mawazo yako na ndoto zako... Mpango ni kutokata tamaa kamwe! Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yeye alipitia na akaja akawa Lejendari huyu tumpendaye na kumheshimu wote.

So nlitaka kumfahamu zaidi, na huwezi kumfahamu mtu kama hujauliza maswali, so tulianzia kwenye asili yake na elimu, na kwa Mama yake ana Baba yake, kwenye kazi yake ya kwanza, vipindi vigumu katika maisha yake, transfer za kazi. Pia jinsi alivyokutana na Mama wa watoto wake, na zaidi tulimzungumzia Mama wa mtoto wake wa pili, wa kwanza hatukumzungumzia, skuona sababu ya kufanya hivyo maana alikua excited zaidi kumuongelea Sarah, ambaye anampikia wali na njegere zilizonyooka zaidi dunia nzima . So alikutana naye vipi? Mwaka gani? Pia tuliongea kuhusu teknolojia na jinsi ambavyo yeye anaenda na wakati. Mahusiano yake na Ivona Kamuntu na AzamTV kwa ujumla.

Kama nilivyosema mwanzo wa story yangu hii na Charles Hillary, naomba ufahamu kwamba hii ni moja ya interview nilizokua natamani kufanya na natumai pia uta enjoy na pia utajifunza chochote kitu kwenye suala zima la utafutaji, malezi, ndoto na mipango maana binafsi nimechota kadhaa. Lejendari akija mezani unachotakiwa kufanya ni kuskiliza zaidi na kuongea kidogo.

Enjoy.

Love,

Salama.

---

Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Oct 15 2020

1hr 14mins

Play

Ep. 37 - Salama Na DR MWAKA | BINGWA

Podcast cover
Read more

Sikuwahi kukutana na Dr Mwaka mimi kabla ya tarehe 26 ya mwezi wa tisa, ila nilishawahi kuongea nae kwa simu mara mbili kabla ya kukutana, hatukuwa marafiki ila maongezi yetu ya mara ya kwanza kwenye simu yalinifanya nijue kwa kiasi yeye ni mtu wa aina gani, na nilivyokutana nae pia iliongeza heshima yangu kwake kwa kazi anayofanya na aina ya mtu yeye alivyo. Nisiseme kwa kupepesa, alini impress na nilijifunza vitu kadhaa kwa muda mchache niliokaa naye na kuongea nae.

Alikuja na mkewe kwenye set ya kipindi na alihakikisha mkewe anafika mpaka kwenye ‘kizuizi’ cha mwisho kabisa kabla ya kufika kwenye meza ya mahojiano na pia alihakikisha macho yake na ya mkewe yanagongana kila anakapopenda kufanya hivyo. Wakati mwengine watu hufanya mambo kwaajili ya camera ili wapate kuongelewa, ila kwa wanaopendana kila kitu huwa kinakua wazi, jinsi wanavyoongea, wanavyocheka, wanavyoangaliana na mengineyo imenipa sababu ya mimi kukubali kwamba wawili hawa ni wanapendana kweli. Na tukumbuke kwamba huyo si mke pekee wa Dr JJ Mwaka kama sote tunavyofahamu, ila hakuna ubishi kwamba yeye pia ni mke wake pendwa kabisa.

Maongezi yetu yalianzia kwenye asili yake kama kawaida, na aina ya maisha anayoishi sasa. Kama ni kipaji au alienda shuleni kusoma haya anayoyafanya, na suala la yeye kuwa Daktari Bingwa wa nguvu za kiume na mambo ya uzazi wa kina Mama, na kama hizo tu ndo tiba yeye hufanya. Alinza lini? Alirithishwa? Na je wakati mwengine maneno watu wanasema juu yake yanamkera au yanampa motisha ya kufanya zaidi? Unaikumbuka ile skendo ya kutaka kufungiwa ofisi? Aliimalizaje? Na chimbuko lake haswa hiyo story ni wapi? Ilikuaje akachomoka humo? Na Kuna khadithi na mahusiano yake na wake zake? Hana mmoja mwenzangu. Anawezaje kukaa na wote? Alishapitia ndoa ngapi? Je kasomea taaluma yake hii? Biashara ina faida? Je kuhusu skendo ya kutumia magonjwa ya wanawake na kujipatia wake ni kweli?

Kusema za ukweli tumeongea sana, na nimejifunza sana kupitia mazungumzo haya na kama ilivyo ada natumai na wewe utaokota mawili matatu na pengine kupata idea ya ajira na kujikwamua kwa hapa na pale. Dr Mwaka pia ni mtu anayependa watu wengine waendelee na aliniambia kama kwa yeye kuja kwenye kipindi kutasaidia hata kwa theluthi tu na kufanya vijana na wengine wajiongeze basi angependa kuja na alifanya hivyo, kwa hilo namshkuru sana. Tafadhali enjoy rafiki.

Love,
Salama.

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Oct 08 2020

1hr 17mins

Play

Ep. 36 - Salama Na JOH MAKINI | KIUNGO

Podcast cover
Read more

Story ya kwanza siku zote itakua ni jinsi ambavyo mimi na Joh Makini tulipokutana mara ya kwanza, nakumbuka vizuuuri sana sana haswa, jinsi alivyokua mwembamba na asiyekua na maneno mengi, ila macho yake, macho yake yalikua kama Askari wa shabaha ambaye akilenga hawezi kukosa, na guess what?

Wanasema katika vitu ambavyo havibadiliki kwa binadamu anapokua basi macho ni moja wapo. Macho yake ni yale yale ya sniper, ila kwa sasa ni ya sniper aliye relax ambaye shabaha zake na malengo yake yanaeleweka. Hahitaji kujitambulisha anapokua kwenye mawindo yake. Heshima zangu nyinyi zinaenda kwake, maana kuweza kukaa kwenye chati toka mwaka 2004/05 mpaka leo hii si jambo ambalo kila muwindaji anaweza kufanya.

So anawezaje? Kipi haswa kinamsukuma mwenzetu huyu kuweza haswa kuendelea na kuwa relevant kiasi hiki? Mimi nimefahamiana naye zamani tu, hiyo miaka ya mwanzo ya 2000 na maendeleo yake na kazi yake kama nilivyosema inajielezea. So swali ni anawezaje au amewezaje? Jengine unalotakiwa kufahamu ni kwamba Mwamba si muongeaji sana. Yeye vitendo ndo zaidi. Na mashairi yake ya kibabe na style laini na nyeusi ndo inamfanya aendelee na yake. Kuweza kuweka kundi la Weusi pamoja na kuwa na discipline ya kazi nayo vipi? Kufanya kazi na mdogo wake ambae ni msomi na kama mwenye maneno mengi wakati mwengine inakuaje? Na yeye na Lord Eyes na GNako walitoana wapi? Sawa wote wametoka Arusha ila huu muungano ulikua wazo la nani? Je ki biashara inawalipa?

Pia tuliongea kuhusu muziki wa sasa, wa ki leo na mbinu ambazo baadhi ya wasanii wanazitumia ili kufikisha ujumbe wao. Mambo yamekua kama mengi ivi, yeye mawazo yake kwenye hizo mbinu ni yepi? Ashawahi kuchanganyikiwa na baadhi ya vitu ambavyo anaviona mtandaoni? Na kama ana wivu?

Kuhusu familia pia nlitaka kuchimbachimba kidogo lakini alikua ngumu maana Joh na familia yake huwa anakua mlinzi haswa. Ni mwaka huu ndo ilikua mara ya kwanza kuona anaweka picha za mwanawe King kwenye Instagram yake. Kwa sababu ambazo yeye anazijua ameamua kufanya hivyo, ya nyumbani ni nyumbani na ya sanaa yake ndo yanaenda mitandaoni. Hapo nilimheshimu sana kwa hilo.

Hip Hop si muziki wa lele mama, ni aina ya muziki wa majigambo haswa na maneno tu peke yake hayakufanyi uwe bora mbele ya wana hip hop wenzako bali uwezo wa kuyatembea unayo yaongea na kukaa juu siku zote za maisha yako ndo heshima hapo inapopatokana, na naamini kwa Joh, hilo hatuna deni nae, au niseme binafsi, SIMDAI. Haya, kama ilivyo kawaida yetu yangu matumaini utapata mawili matatu hapa ya kujisogeza na maisha yako na mipango endelevu, na pengine jinsi ya kutokata tamaa katika maisha na kuamini ndani ya mipango yako na maendeleo yako ndugu yangu. Tafadhali enjoy pia.

Love,
Salama.

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Oct 01 2020

51mins

Play

iTunes Ratings

18 Ratings
Average Ratings
18
0
0
0
0

H

By 4286HP - Apr 29 2020
Read more
Soooo sooo good! I got my whole family to start listening to this podcast!!

Great talk show for East African audience!

By Berry.U - Mar 08 2020
Read more
It’s hard to keep up with legitimate celebrity/pop culture news - especially when living outside of home country,Tanzania...this is a bogas-free platform for getting to know well recognized individuals on a more personal level and learning big life lessons. Thought provoking yet SUPER CHILL! Safi sana 👌🏾👌🏾